MDI kugharamia matibabu ya Neema Makunja
Wazazi wa Neema Makunja mwenye ulemavu wa Miguu hawakumpa fursa ya kujiunga na shule tangu alipofikisha umri wa kupata elimu hiyo kutokana na kile kinachotajwa na wazazi kuwa ni mazingira magumu ya kuifikia shule katika hali yake ya ulemavu.
Baada ya kupata taarifa ya mwananfuzni huyo uongozi wa MDI ulifanya mawasiliano na Hospitali ya CCBRT jijini Dar es Salaam ili kupata ufafanuzi iwapo changamoto hiyo inaweza kupatiwa matibabu.
Baada ya kuthibitishiwa kuwa mlemavu wa aina hiyo anaweza kupatiwa matibabu na kurejea katika hali ya kawaida, MDI imeanzisha michangao kwa ajili ya kumsafirisha kutoka kijijini Kigaga kata ya Nansimo wilayani Bunda kuja Dar es Salaam kwa ajili ya matibabu.
Michango hiyo inalenga kupata milioni 3 ambazo zitawezesha matibabu pamoja na nauli.
Kwa yeyote anayeguswa anaweza kuungana na MDI kwa kufikisha mchangao wake kupitia kwa Bwana Edward Namwata ambaye amepewa jukumu la kukusanya.
Namba yake ni 0757456594

Comments
Post a Comment