Wataalamu Sekta ya maji shirikishaneni maarifa – Naibu Waziri Maji
Naibu Waziri Mhandisi Maryprisca Mahundi
(wa tano kutoka kulia) katika picha ya pamoja mara baada ya kukagua kazi
zinazofanywa na moja ya washiriki kutoka Uholanzi
Mhandisi Mahundi mara baada ya kuzindua Jarida la usimamizi wa rasilimali maji, uhandisi, menejimenti na
sera. Jarida hilo linalenga kuboresha taarifa na kuweka jukwaa la wadau na
wataaluma walio katika sekta ya maji kuchapisha kazi zao za kitafiti.
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi na baadhi ya
wajumbe wa kongamano la Kisayansi la maji
Wajumbe wakiendelea na kongamano katika
ukumbi wa Julius Nyerere jijini Dar es Salaam
Picha ya pamoja ya Mgeni Rasmi na baadhi ya
wajumbe wa kongamano la Kisayansi la maji
Naibu Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca
Mahundi akipata maelezo kwenye moja ya mabanda ya maonesho ya wadau
walioshiriki katika Kongamano la Kisayansi la maji jijini Dar es Salaam
Mhandisi Mahundi akikata utepe kuashiria
uzinduzi wa Jarida la usimamizi wa rasilimali maji, uhandisi, menejimenti na
sera. Jarida hilo linalenga kuboresha taarifa na kuweka jukwaa la wadau na
wataaluma walio katika sekta ya maji kuchapisha kazi zao za kitafiti.
Naibu Waziri wa Maji Mhe. Mhandisi
Maryprisca Mahundi (Mb) amewataka wataalamu na wadau wa sekta ya maji kwa
ujumla kushirikishana ujuzi na taaluma kuweza kutatua changamoto zinazoikumba sekta ya maji kwa
pamoja. Amesema Serikali kupitia Wizara ya Maji itahakikisha inawapa msaada wa
hali na mali ili kuwezesha malengo maalumu ambayo ni pamoja na kumtua mama ndoo
ya maji inafikiwa.
Mhandishi Maryprisca ameyasema hayo wakati
akifungua Kongamano la kisayansi la maji lililofanyika jijini Dar es salaam leo
Aprili 4, 2022. Aidha, Amekipongeza Chuo
cha Maji kwa kuandaa kongamano hilo na kuwa msaada mkubwa katika kuwaandaa
wataalamu wanaohudumu katika sekta ya maji
nchini.
“Uchaguzi wa kauli mbiu ya ‘Usimamizi wa Rasilimali za Maji kwa Huduma Endelevu za Ugavi wa Maji na Usafi wa Mazingira’ katika Kongamano hili imekuwa sambamba na Malengo ya 2025 ya Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ambayo ni ‘kuwezesha upatikanaji wa huduma ya majisafi kwa wote’. Inafurahisha kujua kuwa Kongamano hili linakuwa ni sehemu ya kushirikishana, na kupeana ujuzi katika taaluma na kuleta utatuzi wa changamoto zinazoikumba sekta ya Maji na nyiginezo.” Amesema Mhandisi Mahundi.
Amewataka Chuo cha Maji waendeleze
Kongamano hilo kwa kila mwaka kwani litasaidia kwa kiasi kikubwa kuongeza
maarifa na kuondoa changamoto zinazoikumba sekta ya maji.
Kongamano la Kisayansi la maji limeandaliwa
na Wizara ya Maji kupitia Chuo cha Maji na kuhudhuriwa na mataifa mbalimbali
kutoka nje na ndani ya Afrika. Matokeo ya tafiti zaidi ya 60 yanatarajiwa
kuwasilishwa, huku washiriki zaidi ya 400 wakitarajia kushiriki kwa siku mbili
kuanzia Aprili 4 hadi 5.


.jpeg)


.jpeg)

Comments
Post a Comment