Mhandisi Mshauri atakiwa kusimamia vizuri ili mradi wa maji wa miji 28 ukamilike kwa wakati.
Prosper Buchafwe. Mkurugenzi Sera na Mipango, Wizara ya Maji
Katibu Mkuu Wizara ya Maji Prof. Jamal Katundu amemtaka Mhandisi Mshauri kampuni ya Management Consultant (MC) kuhakikisha wanatoa ushauri wenye tija ili mradi wa maji wa miji 28 utekelezwe na kukamilika kwa wakati.
Agizo hilo amelitoa leo jijini Dodoma kupitia taarifa yake iliyosomwa na Mkurugenzi wa Sera na Mipango, Wizara ya Maji Prosper Buchafwe wakati wa kikao kuhusu utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 kilichofanyika Dodoma.
Prof.Katundu amesema wananchi wanahitaji majisafi, salama na yenye kutosheleza hivyo Mhandisi mshauri anajukumu la kuhakikisha mradi unatekelezwa kwa kuzingatia viwango na ukamilike katika muda uliopangwa na kwamba hilo litawezekana iwapo watakuwa washauri wazuri kwa Menejimenti ya Wizara ili kufanya maamuzi yenye tija.
Ameishukuru Serikali ya India kwa kuwezesha kupatikana kwa fedha za utekelezaji wa mradi huo ambao utapunguza kwa kiasi kikubwa changamoto ya huduma ya maji katika maeneo mbalimbali hapa nchini.
Mradi wa maji wa miji 28 umefadhiliwa na serikali ya India kupitia mkopo wenye masharti nafuu wa dola milioni 500 sawa na zaidi ya shilingi trilioni moja za Tanzania ambazo zitafanikisha mradi huo

Comments
Post a Comment