Maji wakutana kuangalia namna bora ya kuondokana na ukiritimba
Mpango huo unaojulikana pia kama Blueprint, unalenga kuboresha
mazingira ya biashara na uwekezaji nchini kwa kupunguza au kuondoa changamoto
mbalimbali zinazozuia maendeleo ya uwekezaji na biashara.
MKUMBI unalenga kukabiliana na Changamoto hizo kwa kufanya marekebisho ya sheria na kanuni za kisekta, matumizi ya mifumo ya kieletroniki katika kutoa huduma, kuunganisha majukumu ya mamlaka za udhibiti yatakayobainika kuwa na muingiliano; pamoja na uanzishaji wa vituo vya utoaji wa huduma mahali pamoja.
Wizara ya Maji kama sekta muhimu ya kiuchumi na kijamii
ambayo inahusika moja kwa moja na maisha ya wananchi imejipanga na inatambua
umuhimu wa mpango huo katika kuhakikisha uwekezaji unaohusisha huduma ya maji
unarahisishwa, unafikika kwa urahisi na hivyo kusukuma maendeleo ya
taifa.
Kikao kilichofanyika katika ukumbi wa Mamlaka ya Majisafi na Usafi
wa Mazingira mjini Moshi kimewakutanisha wataalamu wa Wizara, Bodi ya Maji
Bonde la Pangani na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mjini Moshi ambao
wamejadiliana masuala mbalimbali ikiwemo
sheria, kanuni na taratibu zinazosimamia utoaji wa vibali vya matumizi ya maji,
hali ya huduma ya maji kwa ujumla na kuweka mikakati ya kuboresha mazingira ya
biashara katika Sekta ya Maji.
Wizara imejipanga kujenga uelewa kwa wadau wa Sekta ya Maji kuhusu
mpango wa MKUMBI kwa lengo la kuvutia uwekezaji endelevu unaozingatia maendeleo
ya Sekta ya Maji.

Comments
Post a Comment