Watumishi sekta ya maji wasisitizwa kutambua nafasi zao katika utoaji wa huduma
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amefanya kikao na Watumishi wa Wizara ya maji mkoani Geita na kuwataka kuzingatia weledi, nidhamu na kuwajibika kwa jamii.
"Kazi hii ya kutoa huduma ya majisafi mkoani Geita ni yetu sote, ni vyema kuipenda na kuifanya kazi hii kwa weledi, bidii na nidhamu Ili kufikia malengo yetu binafsi, taasisi zetu, Wizara na Taifa kwa ujumla" Mhandisi Luhemeja ameainisha.
Amesisitiza watumishi wa Sekta ya Maji kutambua umuhimu wao katika huduma hii muhimu ya kuwafikishia majisafi wananchi wa Geita.
"Nataka wote tujiulize, kazi hii tusipoifanya sisi ataifanya mtu gani mwinginei? Na je tusipompatia mwananchi huyu huduma ya maji nini kitampata?, Majibu ya maswali haya yatatufungua na kuona wajibu wetu katika kuifanya kazi yetu kila siku ya kuihudumia jamii yetu" Mhandisi Luhemeja amesema.
Mhandisi Luhemeja amesisitiza upendo na mshikamano baina ya viongozi na watumishi kama kiungo muhimu kufikia malengo, katika kazi za ofisi na masuala ya jumuiya katika jamii.

Comments
Post a Comment