Serengeti waomba huduma ya maji toka ziwa Victoria
Mbunge wa Jimbo la Serengeti Mhe. Dkt. Amsabi Mrimi akizungumza wakati wa Ziara ya Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja
Chujio la maji Mugumu
Bwawa la Manchira lililoko Wilayani Serengeti
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja amewaagiza wataalam wa Wizara wa Maji kufanya utafiti ndani ya siku tatu wawasilishe taarifa ya namna bora ya kuwezesha upatikanaji endelevu wa huduma ya maji kwa wananchi wa Serengeti.
Ametaka taarifa hiyo baada ya kupokea maelezo ya Mbunge wa jimbo hilo Mhe. Dkt. Amsabi Mrimi kuwa kina cha maji kimepungua kwenye bwawa la Manchira ambalo ni chanzo cha maji cha mradi wa maji wa Mugumu ambao unatarajiwa kuhudumia wakazi wa eneo hilo.
Luhemeja amesema utekekezaji wa mradi huo unaruhusu kusanifu na kujenga hivyo wataalam waje na ushauri iwapo kuna umuhimu wa mradi huo kutumia maji ya Ziwa victoria kupitia mradi wa Tarime-Rorya ambao utekekezaji wake unaendelea.
"Katika Wilaya ya Serengeti wananchi wanatumia maji kutoka bwawa la Manchira kama chanzo cha maji, lakini Mheshimiwa Mbunge anaonesha wasiwasi kwamba inawezekana bwawa hili lisiwe chanzo endelevu kutoa huduma katika eneo hili kutokana na mabadiliko ya tabianchi yanayoathiri ujazo wa maji" Mhandisi Luhemeja amesema
Mhandisi Luhemeja ametoa wito kwa wananchi wa Serengeti kutunza vyanzo vya maji Ili kupunguza athari zinazoweza kukumba vyanzo hivyo.
Aidha Mhe. Dkt. Amsabi ameshukuru Serikali ya awamu ya Sita kwa kutenga fedha kiasi cha shilingi bilioni 20 kuboresha huduma ya maji katika Wilaya ya Serengeti.
"Ongezeko la watu katika Mji huu ni kubwa sana, utalii unakua kwa kasi na maji yanahitajika sana, chanzo tulichonacho kwa sasa bwawa la Manchira limezidi kupungua maji kutoka mita tisa mpaka sita tangu lilipotengenezwa, ni muda sasa wananchi hawa wakapata maji kutoka ziwa Victoria ambacho ni chanzo cha uhakika" Mhe Mrimi ameomba
Mhandisi Wiston Agwaro Kaimu Afisa Maji kutoka Bodi ya Maji Bonde la Ziwa Victoria ameeleza kuwa chanzo cha maji cha Bwawa la Manchira kinatosheleza kwa mahitaji ya sasa.
Amekili kuwepo na changamoto ya mabadiliko ya tabianchi ambayo yanasababisha kupungua kwa maji





Comments
Post a Comment