India waipa Tano sekta ya maji Tanzania.
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Serikali ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyan Jaishankar akisalimiana na Waziri wa Maji wa Tanzania Mhe. Jumaa Aweso wakati wa ziara ya kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo na mfumo wa maji wa Ruvu Juu eneo la Kibamba jijini Dar es Salaam
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso akimkabidhi zawadi Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Serikali ya India. Dkt. Subrahmanyan Jaishankar
Picha ya pamoja na Menejimenti ya DUWASA
Baadhi ya wageni waalikwa wakifuatilia hotuba za viongozi wakati wa Ziara ya Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Serikali ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyan Jaishankar jiji Dar es Salaam
Mhe Aweso
Waziri Mhe. Dkt. Subrahmanyan Jaishankar akizungumza
Waziri wa Mambo ya Nchi za Nje wa Serikali ya India Mhe. Dkt. Subrahmanyan Jaishankar ameipongeza serikali ya Tanzania kwa usimamizi mzuri wa fedha zinazotolewa na serikali hiyo kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maji nchini. Pongezi hizo amezitoa leo Julai 7 alipotembelea na kukagua mradi wa upanuzi wa mtambo na mfumo wa maji wa Ruvu Juu ambao ni moja ya miradi iliyotekelezwa kwa ushirikiano kati ya serikali ya Tanzania na serikali ya India.
Amesema mafanikio ya usimamizi mzuri wa miradi ya maji nchini Tanzania umeipa Imani kubwa serikali ya India na hivyo itaendeleza ushirikiano katika kutekeleza miradi mbalimbali ukiwemo mradi wa miji 24 unao gharimu Dola za Marekani Milioni 500 sawa na takribani shilingi trilioni 1.2 za Tanzania.
Amemtaka Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso afikishe salam hizo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan kwamba serikali ya india inaridhishwa na jitihada za Tanzania katika kuhakikisha utekelezaji wa miradi ya maji unasimamiwa vizuri na thamani ya fedha inaonekana.
Amesema maji ni chakula, maji ni afya, maji ni uhai hivyo mafanikio ya serikali ya Tanzania katika kuwafikishia wananchi huduma ya maji ni mafanikio ya serikali ya India kwa sababu uhusiano wa serikali ya India na Tanzania umekuwepo kwa muda mrefu na utaendelea kuwepo kwa ajili ya ustawi wa wananchi wa pande zote mbili.
Kwa upande wake Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) amemshukuru Waziri huyo na kumhakikishia kuwa serikali ya Tanzania itahakikisha uhusiano mzuri uliopo unaendelezwa. Amesema bado zipo changomoto za huduma ya maji katika mji wa Dodoma na kuiomba serikali ya India iangalie uwezekano wa kushirikiana na Tanzania katika kuondoa changamoto hizo.
“Nikuombe Mheshimiwa Waziri. Serikali imehamia jijini Dodoma. Mahitajhi ya maji katika jiji la Dodoma ni lita milioni 133 kwa siku. Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Dodoma inazalisha lita milioni 67 kwa siku. Ombi langu kwa serikali ya India tushirikiana katika hili ili kuhakikisha jiji la Dodoma linaondokana na changamoto ya huduma ya maji.” Amesema Waziri Aweso.
Baadhi ya miradi ambayo imetekelezwa kwa ushirikiano kati ya Serikali ya Tanzania na Serikali ya India ni pamoja na mradi wa kuboresha huduma ya maji kwa Jiji la Dar es Salaam na Chalinze ambao umetekelezwa kwa gharama ya Dola za Marekani milioni 178.125. Mradi wa maji kutoka ziwa Victoria kwenda katika miji ya Tabora, Igunga, Nzega, Tinde, Uyui, Shinyanga, Shelui na vijiji 102 kwa kiasi cha Dola za Marekani milioni 268.35. Mradi unaoendelea wa miji 24 Tanzania bara na Zanzibar wenye thamani ya Dola za Marekani milioni 500 takribani shilingi trilioni 1.2 za Tanzania






Comments
Post a Comment