Changamoto ya huduma ya majisafi Bunda kufikia kikomo
Wananchi wa Kijiji cha Nyantare wakishangilia baada ya kutembelewa na Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Cyprian Luhemeja
Wakazi wa kijiji cha Nyantare wakimsikiliza Naibu Katibu Mkuu alipowatembelea kijijini hapo
Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amezungunza na wakazii wa mtaa wa Nyantare kata ya Guta na kuwatangazia neema ya majisafi katika makazi yao.
Mhandisi Luhemeja akiwa mkoani Mara amewaambia kuwa lengo la Serikali ifikapo mwaka 2025 ni kuwa kata zote 14 za Wilaya ya Bunda kupata huduma ya majisafi na salama kwa asilimia 98 hadi 100.
"Tunao mradi mkubwa wa maji wa Bunda mjini wenye thamani ya shilingi bilioni 10 na hapa Nyantare tumewafikishia huduma ya majisafi tayari, nimetoa Maagizo kwa Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Bunda kuongeza eneo lake la kihuduma na kuwafikia wananchi wengi zaidi" Mhandisi Luhemeja amesema.
Ameongeza kuwa ameyapokea maombi ya uongizi wa wilaya ya Bunda wa kuwatafutia fedha kwa ajili ya usambazaji wa majisafi kwa wananchi na atakaporudi ofisini ataenda kutafuta kiasi cha shilingi bilioni tano ili huduma ya maji ifike katika makazi ya wananchi.
Mkuu wa Wilaya ya Bunda Mhe. Dk.Vicent Naano ameeleza hali ya upatikanaji wa huduma ya majisafi na salama katika Wilaya ya Bunda kuwa inaimarika na lengo la Serikali kufikia mwaka 2025 kila mwananchi kuwa na huduma ya majisafi Bunda litakamilika.
Naye Haika Muneja mkazi wa mtaa wa Nyantare ameeleza kwa sasa wananafuu kwa kuwa maji yamefika katika mtaa wao kwasababu hapo awali walikuwa na adha kubwa ya kupata huduma ya majisafi.
Katika Hali ya furaha wananchi wa mtaa wa Nyantare walimkaribisha Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja kwa kumkabidhi mtoto mchanga na kumpa jina la Samia ikiwa ishara ya shukrani kwa Mhe.Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuwapelekea majisadi wakazi wa Nyantare.




Comments
Post a Comment