Bilioni 440 Kumaliza changamoto ya majisafi Simiyu.

Naibu katibu Mkuu Mhandisi Cyprian Luhemeja akizungumza na mkandarasi wa mradi

Serikali inatekeleza mradi wa maji wa kukabiliana na mabadiliko ya tabianchi mkoani Simiyu ambao unagharimu shilingi bilioni 440, ambapo mradi utanufaisha wilaya zote za mkoa huo. 

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji, Mhandisi Cyprian Luhemeja amesema hayo mkoani Simiyu wakati akikagua utekelezaji wa miradi ya maji, Pamoja na hali ya utoaji huduma kwa wananchi.

"Mkoa wa Simiyu ni moja kati ya mikoa yenye changamoto ya huduma ya maji kutokana na kutokuwa na vyanzo vya maji, lakini sasa lipo tumaini kubwa. Mhe.Rais Samia ameelekeza shilingi bilioni 440 kumaliza changamoto hii ya maji hapa Simiyu. Hali ya upatikanaji huduma ya maji kwa sasa ni asilimia 71, ila kazi hii ikikamilika upatikanaji wa maji utafika asilimia zaidi ya 95" Mhandisi Luhemeja amebainisha.

Mhandisi Luhemeja ameongeza kuwa Mkandarasi Kampuni ya China Civil Engineering Construction 

Cooperation (CCECC) ipo kazini na wamekubaliana kumaliza kazi hii ifikapo Oktoba 2025 bila kuwa na muda wa ziada. 

Kwa upande wake Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira Vijijini (RUWASA) Mkoa wa Simiyu Mhandisi Mariam Majawa ameeleza kuwa jumla ya Wilaya zote ndani ya Mkoa wa Simiyu zitanufaika na mradi huo ikihusisha idadi ya vijiji vipatavyo 255.

Utekelezaji wa mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi Simiyu ni moja ya  nia ya dhati ya Serikali ya Awamu ya sita katika kumaliza na kutatua kero za majisafi kwa wananchi  nchini kote.

Comments

Popular posts from this blog

Ujenzi wa Mabwawa kusaidia kuondoa changamoto ya maji Dodoma

Wataalamu Sekta ya maji shirikishaneni maarifa – Naibu Waziri Maji

Katibu Mkuu Wizara ya Maji asisitiza matumizi ya mfumo wa taarifa za sekta ya maji (Maji App)