Eng. Kemikimba aongoza ujumbe wa Tanzania Mkutano Kamati ya Pamoja ya Kisera

Picha za pamoja za Mkutano wa Kumi wa Kamati ya Pamoja ya Kisera ya Makatibu Wakuu ya Usimamizi wa Miradi na Program zinazotekelezwa kupitia kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ambao umefanyika nchini Kenya

Naibu Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Nadhifa Kemikimba kwa niaba ya Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga ameongoza ujumbe wa Tanzania kwenye Mkutano wa Kumi wa Kamati ya Pamoja ya Kisera ya Makatibu Wakuu ya Usimamizi wa Miradi na Program zinazotekelezwa kupitia kamisheni ya Bonde la Ziwa Victoria ambao unafanyika nchini Kenya kuanzia Februari 2 - 3, 2023 . 

Miongoni mwa mambo muhimu yaliyo jadiliwa ni pamoja na Program Shirikishi katika ya Usimamizi wa Rasilimali za Maji, Mradi wa Kikanda wa Majaribio Kuhimili Mabadiliko ya Tabia ya Nchi Pamoja na Mradi wa kuboresha kilimo chenye uhimilivu kupitia Ziwa Victoria.

Miradi na program hizo zenye faida kubwa kwa Tanzania ni pamoja na kupanua miundombinu ya majitaka katika jiji la Mwanza  chini ya Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA) utakaogharimu Euro Milioni 5.3, kukabiliana na mabadiliko ya tabia nchi na kuimalisha huduma za ulinzi, mawasiliano, usalama wa usafirishaji pamoja na uokoaji katika Ziwa Victoria kwa mkoa wa Mwanza na kituo kidogo cha Entebble nchini Uganda

Mkutano huo ulijumuisha ofisi ya Makamu wa Rais - Mazingira, Wizara ya Fedha na Mipango, Wizara ya Maji, Wizara ya Uchukuzi na Mawasiliano, Shirika la Uwakala wa Meli Tanzania, Bodi ya Maji Ziwa Victoria na Mamlaka ya Majisafi na Usafi wa Mazingira Mwanza (MWAUWASA)

Comments

Popular posts from this blog

Ujenzi wa Mabwawa kusaidia kuondoa changamoto ya maji Dodoma

Wataalamu Sekta ya maji shirikishaneni maarifa – Naibu Waziri Maji

Katibu Mkuu Wizara ya Maji asisitiza matumizi ya mfumo wa taarifa za sekta ya maji (Maji App)