Dkt. Mpango awataka wataalam kusimamia utunzaji wa vyanzo vya maji

 

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango ameshudia uwekwaji saini wa azimio la Mbeya katika uzinduzi wa kampeni ya kitaifa ya Upandaji Miti Rafiki wa Maji na Ufunguzi wa Mkutano Mkuu wa Nane wa Mwaka wa Bodi za Maji za Mabonde uliofanyika jijini humo.

Azimio hilo lilisainiwa na Mawaziri wa sekta mtambuka na linalenga kuhifadhi, kutunza na kuendeleza rasilimali za maji.

Akizungumza baada ya kusaini mikataba hiyo Mhe. Mpango amewataka viongozi wa Vyama vya Siasa na Wataalamu wa sekta zote kusimamia kikamilifu, kuweka mipaka, na kuwaondoa wananchi waliojenga maeneo ya milima mbayo ni vyanzo vya maji kwa kuwahamishia maeneo mengine.





 

Comments

Popular posts from this blog

Ujenzi wa Mabwawa kusaidia kuondoa changamoto ya maji Dodoma

Wataalamu Sekta ya maji shirikishaneni maarifa – Naibu Waziri Maji

Katibu Mkuu Wizara ya Maji asisitiza matumizi ya mfumo wa taarifa za sekta ya maji (Maji App)