Katibu Mkuu Maji awataka 'Maji Sport' kuleta vikombe mashindano ya SHIMIWI
Viongozi wa Klabu ya Michezo ya Wizara ya Maji (Maji Sports Club) wakiongozwa na Makamu Mwenyekiti wa Club hiyo Andrew Rutta wamefika ofisini kwa Katibu Mkuu Wizara ya Maji Mhandisi Anthony Sanga kwa dhumuni la kujitambulisha na kumpa maendeleo ya Klabu hiyo.
Katibu Mkuu Amewapongeza kwa utayari wao wa kushiriki mashindano. Amesisitiza kuwa suala la michezo ni muhimu kwa Wizara ya Maji ambayo ina jukumu la kuwapelekea wananchi huduma ya majisafi na salama. Michezo inasaidia kuleta umoja, afya na inajenga uzalendo na mshikamano.
Amewataka washiriki wawe na nidhamu ili kufikia lengo lililokusudiwa, wasiwagawe watumishi, michezo isiwe uadui iwe ni furaha na kujenga umoja na mshikamano uliokusudiwa.
Klabu ya
Maji inajiandaa kwa ajili ya mashindano ya Shirikisho la Michezo ya Wizara na Taasisi za Serikali
(SHIMIWI) yanayotarajiwa kufanyika Jijini Tanga kuanzia Agost 1, mwaka huu.
Comments
Post a Comment