Aweso awataka wananchi wasiamini ushirikina katika sayansi ya maji
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso (Mb) akizungumza na wananchi wa kijiji cha Wiyenzele Wilayani Mpwapwa mkoani Dodoma wakati wa ziara ya kikazi kukagua utekelezaji wa mradi wa maji katika kijiji hicho.jpeg)
Mmoja wa wananchi wa Kijiji cha Wiyenzele akiwasilisha hoja kwa Waziri
Waziri wa Maji Mhe. Jumaa Aweso ((Mb) ametembelea mradi wa
maji wa kijiji cha Wiyenzele Wilaya ya Mpwapwa mkoani Dodoma na kumuagiza
Meneja wa Wakala wa Maji na Usafi wa
Mazingira Vijijini (RUWASA) wilayani Mpwapwa Mhandisi Cyprian Warioba
kuhakikisha ndani ya siku 30 anatanzua changamoto kuhusu kukamilika kwa mradi
huo.
Mhe. Aweso ametoa kauli hiyo baada ya kupokea malalamiko ya
wananchi kuhusu mradi huo uliokamilika mwaka 2016, na mwaka 2020 mradi huo ulipata changamoto ya
kuharibika kwa pampu.
Wamesema matengenezo ya pampu hiyo yamekuwa yakifanyika
kupitia wakandarasi tofauti tofauti bila mafanikio.
Baada ya matengenezo hayo kushindikana, pampu mpya
ilinunuliwa lakini bado huduma haijarejeshwa.
"Niwaombe radhi
wananchi. Tusitafute mchawi. Hawa wataalamu
wetu ndio wanatakiwa kutumia maarifa yao kutekeleza mradi huu kwa kuzingatia
hali ya udongo wa eneo hili.
Nawaagiza mbele yenu. Ndani ya mwezi mmoja changamoto zote
za eneo hili zipatiwe ufumbuzi. Maji yaanze kutoka." Waziri Aweso amesema.
Kwa upande wake Mbunge wa jimbo la Kibakwe ambako kijiji
hicho kinapatikana Mhe. George Simbachawene (Mb) ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi
ya Waziri Mkuu Sera, Bunge na Uratibu amewataka wananchi waiamini Serikali,
waache kukimbilia imani za kishirikina badala yake wakae pamoja na wataalamu wa
Wizara ya Maji, washirikiane na viongozi wa dini na wazee mashuhuri kuhakikisha
changamoto zilizopo zinapatiwa ufumbuzi.
.jpeg)
.jpeg)
.jpeg)

Comments
Post a Comment