Kongamano la Kisayansi la Kimataifa kufanyika Dar Es Salaam
Mkuu wa Chuo cha Maji Dkt. Adam Karia akizungumza na Waandishi
wa Habari kuhusiana na Kongamano la Kisayansi la Maji linalotarajiwa kufanyikia
kwa siku mbili kuanzia kesho Aprili 4-5 katika Kituo cha Mikutano cha Kimataifa
cha Julius Nyerere jijini Dar es Salaam. Mgeni Rasmi katika kongamano hilo ni Naibu
Waziri wa Maji Mhandisi Maryprisca Mahundi.
Dkt. Karia amesema wadau wa sekta ya maji zaidi ya 400
kutoka sehemu mbalimbali Duniani wanatarajia kushiriki. Aidha, matokeo ya tafiti
zaidi ya 60 zenye lengo la kuleta matokeo chanya katika kutatua changamotop za
sekta ya maji nchini zinatarajiwa kuwasilishwa.




Comments
Post a Comment